Latest Blog

Latest From Our Blog

Kushirikiana na Wakulima, Kujenga Kilimo Bora!
Seedland Aug 22, 2026
Kushirikiana na Wakulima, Kujenga Kilimo Bora!

Afisa Kilimo kutoka Seedland akiwa katika kikao na wakulima wa AMCOS ya Wino, Mkoa wa Ruvuma, akiwapatia elimu na uelewa kuhusu bidhaa za Seedland, matumizi sahihi ya mbegu na kanuni bora za uzalishaji. Tunazidi kusogeza maarifa, teknolojia na mbegu bora karibu na mkulima ili kuongeza tija na mavuno. SEEDLAND – PANDA UVUNE ZAIDI!

Mkurugenzi wa TOSCI Atembelea Banda la Seedland!
Seedland Aug 8, 2026
Mkurugenzi wa TOSCI Atembelea Banda la Seedland!

Mkurugenzi wa TOSCI Atembelea Banda la Seedland! Tumepata heshima ya kumpokea Mkurugenzi wa TOSCI katika banda letu la Seedland kwenye Maonesho ya Nane Nane 2026. Ametembelea pia vitalu vyetu vya maonesho, akishuhudia kwa vitendo ukuaji na ubora wa mbegu zetu. Ameonesha kufurahishwa na kazi kubwa inayofanywa na Seedland katika kuhakikisha wakulima wanapata mbegu bora kwa kilimo chenye tija. Seedland – Panda Mbegu Bora, Vuna Zaidi!

Karibu Siku ya 7 ya Maonesho ya Nane Nane 2026!
Seedland Aug 7, 2026
Karibu Siku ya 7 ya Maonesho ya Nane Nane 2026!

Karibu Siku ya 7 ya Maonesho ya Nane Nane 2026! Tunaendelea kuwakaribisha wakulima, wadau wa kilimo na wageni mbalimbali kwenye banda la Seedland.

Ugeni wa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Mipango na Uwekezaji
Seedland Aug 6, 2026
Ugeni wa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Mipango na Uwekezaji

Seedland Yapokea Ugeni wa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Mipango na Uwekezaji Tumepata heshima ya kutembelewa na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Mipango na Uwekezaji, Dkt. Pius Chaya, katika banda letu la Seedland kwenye Maonesho ya Nane Nane 2026. Katika ziara hiyo, Dkt. Pius Chaya ameweza kujionea huduma zetu, bidhaa mbalimbali za mbegu bora tunazozalisha, pamoja na juhudi za Seedland katika kuunga mkono ukuaji wa sekta ya kilimo nchini. Ametoa pongezi kwa ubora wa mbegu zetu na mchango wetu katika kuwawezesha wakulima kupata mavuno bora na kuongeza tija katika kilimo. Tunashukuru kwa kututembelea na kutupa moyo wa kuendelea kutoa suluhisho bora kwa wakulima wa Tanzania.

Mkurugenzi wa Huduma TARURA Atembelea Banda la Seedland
Seedland Aug 6, 2026
Mkurugenzi wa Huduma TARURA Atembelea Banda la Seedland

Mkurugenzi wa Huduma TARURA Atembelea Banda la Seedland Tumepata heshima ya kutembelewa na Mkurugenzi wa Huduma wa TARURA, Bi. Azimina Mbilinyi, katika banda letu la Seedland wakati wa Maonesho ya Nane Nane 2026. Bi. Azimina Mbilinyi amefurahishwa na ubora wa mbegu zetu, ubunifu wa bidhaa pamoja na huduma tunazowapatia wakulima. Kutokana na kuvutiwa na ubora huo, ameweza kuchukua aina mbalimbali za mbegu za Seedland kwa ajili ya matumizi na majaribio.

Seedland Yatembelewa na Songea AMCOS!
Seedland Aug 4, 2026
Seedland Yatembelewa na Songea AMCOS!

Seedland Yatembelewa na Songea AMCOS! Tunayo furaha kubwa kuwapokea wanachama wa Songea AMCOS waliotutembelea katika banda letu la Seedland wakati wa Maonesho ya Kilimo Biashara Nane Nane 2026. 🇹🇿 Walipata nafasi ya kujifunza zaidi kuhusu mbegu zetu bora za mahindi (T630 & T416) na alizeti (Seedland 88 & Seedland 77), pamoja na teknolojia na mbinu zinazosaidia wakulima kuongeza uzalishaji na kupata mavuno yenye tija. Tunawashukuru sana Songea AMCOS kwa kututembelea na kushirikiana nasi katika kujenga kilimo chenye mafanikio nchini Tanzania



Events

Upcoming Events

No upcoming events

Check back soon for upcoming events!



Frequently Asked Question

You May Ask

Yes, we supply certified high-yield seeds for various crops.
We conduct regular workshops and field days for farmers.
Yes, we have an established export network and can facilitate market access.
We have both conventional and certified organic product lines.
We manage farms across the fertile highlands and coastal regions.

My Cart

Your cart is empty

 

 

Resolving Details