Seedland Yatembelewa na Songea AMCOS!
Tunayo furaha kubwa kuwapokea wanachama wa Songea AMCOS waliotutembelea katika banda letu la Seedland wakati wa Maonesho ya Kilimo Biashara Nane Nane 2026.

Walipata nafasi ya kujifunza zaidi kuhusu mbegu zetu bora za mahindi (T630 & T416) na alizeti (Seedland 88 & Seedland 77), pamoja na teknolojia na mbinu zinazosaidia wakulima kuongeza uzalishaji na kupata mavuno yenye tija.
Tunawashukuru sana Songea AMCOS kwa kututembelea na kushirikiana nasi katika kujenga kilimo chenye mafanikio nchini Tanzania
Leave a Comment