
Seedland Yapokea Ugeni wa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Mipango na Uwekezaji
Tumepata heshima ya kutembelewa na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Mipango na Uwekezaji, Dkt. Pius Chaya, katika banda letu la Seedland kwenye Maonesho ya Nane Nane 2026.
Katika ziara hiyo, Dkt. Pius Chaya ameweza kujionea huduma zetu, bidhaa mbalimbali za mbegu bora tunazozalisha, pamoja na juhudi za Seedland katika kuunga mkono ukuaji wa sekta ya kilimo nchini.
Ametoa pongezi kwa ubora wa mbegu zetu na mchango wetu katika kuwawezesha wakulima kupata mavuno bora na kuongeza tija katika kilimo.
Tunashukuru kwa kututembelea na kutupa moyo wa kuendelea kutoa suluhisho bora kwa wakulima wa Tanzania.
Leave a Comment